13 Machi 2015 - 11:34
Mwanachama mwandamizi wa Al-Shabaab auawa Somalia

Inasadikiwa kuwa mwanachama mwandamizi wa kundi la Al-Shabaab, Adan Garar, ameuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani nchini Somalia.

Inasadikiwa kuwa mwanachama mwandamizi wa kundi la Al-Shabaab, Adan Garar, ameuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani nchini Somalia. Maafisa wa Kenya na Marekani wamesema inaaminiwa Garar na watu wengine wawili wameuawa baada ya gari lao kushambuliwa karibu na mji wa Bardhere. Garar anatuhumiwa kusaidia kupanga mashambulizi ya kigaidi katika jengo la biashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya mwaka 2013 na kusababisha mauaji ya watu 67. Garar pia anashutumiwa kupanga mashambulizi yaliyoshindikana katika pwani ya Kenya na mji mkuu wa Uganda, Kampala mwaka uliopita.